Andrew Komba

Facebook wakubali kwamba matumizi ya mtandao huo yana madhara kwa maisha ya kila siku

By  
Facebook-wakubali-kwamba-matumizi-ya-mtandao-huo-yana-madhara-kwa-maisha-ya-kila-siku


Mkurugenzi wa tafiti Facebook David Ginsberg na mtaalamu wa utafiti Moira Burke wamekubali kwamba matumizi ya mtandao wa Facebook unamadhara makubwa sana kwenye jamii. Viongozi hao wa ngazi za juu kwenye kampuni hiyo ya Facebook walikubali madhara ya mtandao huo kwenye jamii kutokana na maswali mengi kuwepo dhidi ya madhara ya mtandao huo kwenye jamii.

Katika utafiti uliofanywa, unaonesha kwamba watu wanaotumia mtandao huo kuangalia machapisho ya watu wengine huwa wanakuwa katika hali ya msongo wa mawazo, wakati wale wengine wanaotumia mtandao huo kuchapisha na kuwasiliana na marafiki wanakuwa katika hali ya furaha.

Hii inamaana kwamba kama unatumia muda wako mwingi Facebook kuangalia news feed au ku like machapisho ya watu, lazima utakuja kusumbuliwa na msongo wa mawazo.

Facebook pia walishirikiana na chuo cha Carnegie Mellon katika kutambua zaidi tabia za watu ndani ya mtandao huo, na kugundua "watu wanaotumia mtandao huo kuwasiliana, kutoa maoni, na kuchapisha vitu, huwa ni wale ambao wanafuraha sana, wasiokuwa na msongo wa mawazo." Pia utafiti huo ulionesha kwamba watu wanaotumia dakika 5 kuangalia Profile zao huwa wanajikubali sana tofauti na wale ambao wanaangalia profile za watu wengine.

Tunahitimisha kwa kusema Facebook imetengenezwa maalum kwa kuwasiliana na watu wengine, na ukifanya hivyo ndo inashauliwa na ni nzuri kiafya, ila kama utatumia mtandao huo kivingine basi utakuwa ni mlengwa wa madhara kama msongo wa mawazo, upweke, ambapo si nzuri kiafya.


ANGALIA HII VIDEO: MAKOSA 10 AMBAYO VIJANA WENGI WANAFANYA WAKATI WA USAILI WA KAZI

SOMA ZAIDI
Andrew Komba

Jinsi Ya Kumjua Mtu Aliyekataa Ombi Lako La Urafiki Facebook

Jinsi-Ya-Kumjua-Mtu-Aliyekataa-Ombi-Lako-La-Urafiki-Facebook


Kama ni mtumiaji wa Facebook basi lazima utakuwa unafahamu jinsi inavyokera unapokuwa unamsubilia mtu akubali ombi lako la urafiki ulilomtumia. Ila kuna njia ambayo unaweza ukatambua kama mtu huyo na wengine wote uliowaomba urafiki kama wamekubali au ndo wamekataa ombi lako.

Leo tutakwenda kukuonesha namna ya kujua kama mtu amekubali au amekataa ombi lako la urafiki Facebook.

Fungua akaunti yako ya Facebook kisha bonyeza kwenye ikoni ya "Friends" upande wa kulia juu.

Fungua-akaunti-yako-ya-Facebook-kisha-bonyeza-kwenye-ikoni-ya-Friends-upande-wa-kulia-juu

Bonyeza hapo chini walipoandika "See All."

Bonyeza-hapo-chini-walipoandika-See-All.

Kisha bonyeza hapo juu walipoandika "View Sent Request."

Kisha-bonyeza-hapo-juu-walipoandika-View-Sent-Request.

Sasa hapo utaona orodha ya watu wote ambao hawajakubali ombi lako la urafiki.

Sasa-hapo-utaona-orodha-ya-watu-wote-ambao-hawajakubali-ombi-lako-la-urafiki.

Hapo utakuwa umefahamu watu wote ambao wamekataa ombi lako la urafiki, na unaweza ukaghairisha maombi hayo ya urafiki kwa kuambaisha kishale juu ya "Friend Request Sent" kisha bonyeza hapo chini walipoandika "Cancel Request."

Tuandikie maoni yako kuhusu chapisho hili kwenye ukurasa wetu wa Facebook, pia usisahau kusubscribe channel yetu ya YouTube kwa video zilizochambuliwa kwa undani zaidi juu ya masuala yanayotokea Duniani.

INAYOTAZAMWA SASA: KITANDA HIKI KINAWEZA BADILIKA KUWA SEHEMU YA KUANGALIZIA SINEMA

SOMA ZAIDI
Andrew Komba

Kutumia Simu Au Kompyuta Kwa Muda Mrefu Ni Mbaya Sana Kwako

By  
Kutumia-Simu-Au-Kompyuta-Kwa-Muda-Mrefu-Ni-Mbaya-Sana-Kwako


Hakuna asiyefahamu madhara yanayoweza sababishwa na matumizi ya kompyuta au simu kwa muda mrefu lakini wengi wetu tumekuwa tukipuuza na kuendelea kutumia vifaa hivyo kwani vimekuwa kama sehemu ya maisha yetu, kwa sababu kupitia vifaa hivyo kama tv na simu tunaweza kupata habari mbali mbali kwa urahisi huku kompyuta zikitusaidia kufanya shughuli zetu za kiofisi, na kuna baadhi ya watu wanalazimika kutumia kompyuta kwa siku nzima kutokana na shughuli zao kuwataka kufanya hivyo ili kujitengenezea kipato huku vijana siku hizi simu za mkononi ndiyo imekuwa sehemu ya maisha yetu kwani hatuwezi kukaa hata dakika kadhaa pasipo kuangalia nini kimetokea kwenye ulimwengu wa mitandao.

Ukweli ni kwamba kama unaangalia kompyuta, simu, tv, au chombo kingine chochote cha kielektroniki chenye skrini kwa zaidi ya masaa saba kwa siku, basi tambua lazima utakuja kuwa na matatizo ya macho huko uzeeni kwako. Sasa hapo unaweza ukasema kwamba ni ule mwanga unaotoka kwenye vifaa hivyo ndiyo tatizo kubwa lakini si kweli tatizo ni machozi yaliyokuwa kwenye macho.

Machozi kivipi.

Machozi yanakazi kubwa sana kwenye macho na sote tunayapenda machozi ukiachilia mbali katika kuonesha hisia za mtu, ila machozi kwenye macho yanakazi kubwa sana, kama kuhakikisha macho yetu yana kuwa masafi muda wote pamoja na kuyalainisha. Sehemu muhimu katika mfumo wa machozi ni kope za macho. Pindi mlija wa machozi unaofahamika kitaalamu kama Nasolacrimal Duct au Tear Duct ukiwa unahifadhi machozi kwenye kingo za macho yetu, machozi hayo hujaa. Hivyo kama tukikopesa macho, tunasaidia kusambaza machozi hayo katika jicho zima na kusaidia kuliweka jicho katika hali ya usafi, yaani ni kama windshield inavyosafisha kioo cha gari.

Sasa, kivipi hii inahusiana na kuangalia kompyuta, tv, au simu kwa muda mrefu.

Unapokuwa unaangalia kompyuta, simu, au tv kwa muda mrefu macho huwa yanakopesa kwa muda mchache sana, pamoja na kutanuka kuliko kawaida na hii inasababisha machozi yanayolainisha jicho kukauka haraka sana kutokana na kukodoa kwa muda mrefu, hivyo hupelekea mtu kupata ugonjwa wa kukauka macho Dry Eye Sydrome.

Hivyo basi, kama unajua ni vigumu kwako kukaa mbali na kompyuta, simu, au tv unaweza ukafanya mambo haya yafuatayo ili kuokoa macho yako:

  • Hakikisha unapumzika kutumia kifaa chako (Simu, kompyuta, au tv) walau kila baada ya dakika 30
  • Hakikisha skrini inakuwa chini yako, yaani uwe unaangalia kwa chini, hii itasababisha macho yako yawe yanakopesa kidogo.
  • Epuka kukaa sehemu ambazo hewa inapuliza kwa kasi, kama chini ya AC au karibu na feni
  • Hakikisha eneo ulipo kuna hewa ya uvuguvugu kidogo

Tuandikie maoni yako kuhusu chapisho hili kwenye ukurasa wetu wa Facebook, pia usisahau kusubscribe channel yetu ya YouTube kwa video zilizochambuliwa kwa undani zaidi juu ya masuala yanayotokea Duniani.

INAYOTAZAMWA SASA: KITU ALICHOFANYA MWANAMITINDO HUYU SIO CHA KAWAIDA

SOMA ZAIDI
Andrew Komba

Hivi Ndivyo Kompyuta Zitakavyotawala Binadamu Duniani

By  
Hivi-Ndivyo-Kompyuta-Zitakavyotawala-Binadamu-Duniani

Nadhani wengi wetu tutakuwa tumeshawahi kuangalia filamu maarufu kama Terminator iliyochezwa na Arnold, na zingine nyingi ambazo zenye maudhui ya kuonesha jinsi kompyuta zenye weledi wa hali ya juu zikiiteka Dunia na kutaka kuangamiza binadamu wote. Kutokana na kukua kwa kasi kwa teknolojia ya kompyuta zenye weledi wa hali ya juu (Artificial Intelligence) wanasayansi kutoka sehemu mbali mbali Duniani wanaamini ndani ya miaka 100 kutokea sasa, Dunia yetu itakuwa imetawaliwa na kompyuta hizo zenye weledi wa hali ya juu ambapo hazitakuwa tofauti kimaumbo na binadamu ila kwa akili zitakuwa zimetuzidi sana.

Dunia-yetu-itakuwa-imetawaliwa-na-kompyuta-hizo-zenye-weledi-wa-hali-ya-juu
Muonekano wa roboti zenye weledi wa hali ya juu kiakili / picha kutoka kwenye filamu ya iRobot
Hivi karibuni yaliyoteka malumbano makali sana kati ya mabilionea wawili Mark Zuckerberg ambaye ni muanzilishi wa mtandao kijamii wa Facebook, pamoja na mmiliki wa kampuni ya Tesla, Elon Musk, mabishano yao makali ambayo yalikuwa ni kuhusu madhara ambayo yanaweza kuletwa kutokana na kuziboresha kompyuta kiuwezo wa akili, ambapo bwana Elon Musk akipingana na muendelezo wa teknolojia hiyo ya Artificial Intelligence wakati Mark Zuckerberg akisema haina madhara kwani tangu kuzinduliwa kwake teknolojia hiyo imeleta msaada mkubwa sana kwenye taasisi na mashirika mbali mbali mfano kusaidia kufanya upasuaji mahospitalini kwa wagonjwa na kwenye nyanja ya magari yanayojiendesha yenyewe. Mjadala huo dhidi ya mabilionea hao wawili uliishia kwa Elon Musk kumwambia Mark Zuckerberg ufahamu wake dhidi ya teknolojia hiyo ni mdogo sana hivyo hawezi tambua madhara yake.

Mark-Zuckerberg-na-Elon-Musk-wamekuwa-wakibishana-vikali-kuhusu-Artificial-Intelligence
Kushoto ni Mark Zuckerberg wa Facebook na kulia ni Elon Musk wa Tesla
Artificial Intelligence ni nini? Artificial Intelligence ni tawi la sayansi ya kompyuta ambapo dhumuni kubwa la teknolojia hiyo ni kuunda kompyuta zenye uwezo mkubwa wa kiakili kama kutatua matatizo mbali mbali pasipo kutegemea binadamu, kutafakari, kujifunza, kupanga mikakati, kujitambua zenyewe pamoja na uwezo wa kufanya kazi kama binadamu.

Mpaka kufikia sasa baadhi ya kazi nyingi za viwandani kwenye nchi zilizoendelea zinafanywa na maroboti mfano uundwaji wa magari, na upakiaji wa vitu kwenye viwanda vikubwa. Inategemewa ndani ya miongo miwili ijayo kazi nyingi zitachukuliwa na maroboti na kuacha idadi kubwa ya watu bila kazi.

kazi-nyingi-zitachukuliwa-na-maroboti
Sehemu kubwa ya nguvu kazi itachukuliwa na maroboti
Mwanasanyansi Stephen Hawking na Elon Musk wamekuwa mstari wa mbele kupinga muendelezo wa teknolojia ya Artificial Intelligence, huku hofu kubwa iliyokuwepo kwa wanasayansi hao pamoja na mijadala mikali inayofanywa na wataalam wa masuala ya teknolojia Duniani kote, ni kwamba kukua kwa kasi kwa teknolojia hiyo kunaweza kusababisha mwisho wa Dunia, ambapo hapo baadae kompyuta zitakuwa na uwezo mkubwa wa kiakili hivyo kututawala sisi binadamu kama binadamu wanavyotawala wanyama wengine majumbani kama mbwa, ng'ombe n.k.

wanadamu-watakuwa-ni-watumwa-wa-maroboti
Picha sanifu ya Artificial Intelligence
Mwanzoni mwa mwaka huu kampuni ya Facebook walilazimika kuzima moja kati ya kompyuta iliyokuwa na uwezo wa Artificial Intelligence, sakata hilo lilitokea baada ya kompyuta hiyo kuweza kutengeneza lugha yake yenyewe ambayo hakuna binadamu aliyekuwa anaielewa lugha hiyo, hivyo wasiwasi mkubwa ulitanda kwamba huenda kompyuta hiyo ikiendelea kuachwa basi inaweza ikatengeneza lugha ambazo zikatumika katika mawasiliano dhidi ya maroboti na binadamu hatutoweza kuzielewa. Tahadhari kubwa ilichukuliwa na kompyuta hiyo ilizimwa haraka sana.

Tuandikie maoni yako kuhusu chapisho hili kwenye ukurasa wetu wa Facebook, bila kusahau kusubscribe channel yetu ya YouTube kwa habari, makala, na mambo mengi sana yanayotokea kila siku.INAYOTAZAMWA SASA: JE, UNATAKA KUTENGENEZA KIPATO CHA ZIADA MTANDAONI TEMBELEA TOVUTI HIZI TANO KUFAHAMU

SOMA ZAIDI
Andrew Komba

Vifahamu Vyombo Pekee Kuwahi Kutengenezwa na Binadamu Ambavyo Vimetoka Nje Ya Mfumo Wetu Wa Jua

By  

Vifahamu-Vyombo-Pekee-Kuwahi-Kutengenezwa-na-Binadamu-Ambavyo-Vimetoka-Nje-Ya-Mfumo-Wetu-Wa-Jua


Mwaka 1977 shirika la NASA kutoka nchini Marekani ambalo linahusika na uundaji wa ndege za kisasa pamoja na safari za anga ya nje, walitengeneza vyombo viwili vilivyofahamika kama Voyager 1 na 2 ambavyo viliundwa kwa ajili ya kufanya safari za ndani zaidi kwenye anga la nje.

Chombo cha kwanza kuruka kilikuwa ni Voyager 2, ambacho kilirushwa tarehe 20/08/1977 na kufuatia kingine kilichoitwa Voyager 1, ambacho kilirushwa tarehe 05/09/1977. Vyombo hivyo viwili ambavyo kila kimoja kilirushwa kwenye njia yake, huku Voyager 1 kilitakiwa kufikia sayari ya Sumbula na Zohari, kabla ya Voyager 2.

Chombo-cha-kwamza-kuruka-kilikuwa-ni-Voyager-2
Roketi ikionekana pichani kuipeleka Voyager 2 angani
Pichani hapo chini ni moja kati ya kamera ambayo imefungwa kwenye chombo cha Voyager 2, ikioneshwa na Richard Laeser ambaye ni mkurugenzi wa safari za Voyager 1 na 2.

Pichani-hapo-chini-ni-moja-kati-ya-kamera-ambayo-imefungwa-kwenye-chombo-cha-Voyager-2,-ikioneshwa-na-Richard-Laeser-ambaye-ni-mkurugenzi-wa-safari-za-Voyager-1-na-2
Pichani mkurugenzi wa safari za Voyager 1 na 2 Richard Laeser akizungumzia juu ya kamera iliyofungwa kwenye voyager 2
Wahandisi wakiunda antena kubwa ambayo ilikwenda kutumika kwenye moja kati ya vyombo vya Voyager 1 na 2.

Wahandisi-wakiunda-antena-kubwa-ambayo-ilikwenda-kutumika-kwenye-moja-kati-ya-vyombo-vya-Voyager-1-na-2
Pichani wahandisi wakiunda moja kati ya antena za kwenye Voyager
Voyager 1 na 2 vimewekewa rekodi mbili za dhahabu ambazo zinasauti mbali mbali kutoka Duniani, ikiwemo sauti za salamu za watu kutoka lugha 60 tofauti tofauti, miziki ya tamaduni mbali mbali, sauti za watu wakiongea, wanyama, magari, ndege na vyombo vingine vya usafiri.

Voyager-1-na-2-vimewekewa-rekodi-mbili-za-dhahabu-ambazo-zinasauti-mbali-mbali-kutoka-Duniani
Pichani rekodi mbili za dhahabu ambazo zimebeba sauti na picha mbali mbali kuhusu Dunia yetu
Hii ni picha ya kwanza ambayo ilipigwa na Voyager 1 tarehe 18/09/1977 wakati chombo hicho kilipokuwa umbali wa maili milioni 7.25 (kilomita milioni 11.66) kutoka Duniani.

Hii-ni-picha-ya-kwanza-ambayo-ilipigwa-na-Voyager-1
Picha ya muonekano wa Dunia na mwezi iliyopigwa na voyager 1
Hii picha ilipigwa tarehe 05/03/1979 wakati Voyager 1 ikiikaribia sayari ya Sumbula.

Hii-picha-ilipigwa-na-Voyager-1-wakati-ikiikaribia-sayari-ya-Sumbula
Voyager 1 ikiikaribia sayari ya Sumbula / picha ilipigwa na voyager 1
Kati ya mwezi Januari na Februari mwaka 1979, chombo cha Voyager 1 kilisogea kwa ukaribu kwenye sayari ya Sumbula na kuweza kunasa picha kadhaa ambazo zilionesha uso wa sayari hiyo kwa ukaribu, ikiwamo mawingu yake ya gesi pamoja na kimbunga kikubwa sana kwenye mfumo wetu wa Jua (Our Solar System). Kimbunga hicho kinafahamika kama The Great Red Spot ambacho upepo wake unavuma maili 400 kwa saa huku kikiwa kinazunguka kwenye sayari hiyo, na ukubwa wa kimbunga hicho ni sawa na Dunia zetu tatu.

Kimbunga-hicho-kinafahamika-kama-The-Great-Red-Spot
Muonekano wa karibu wa sayari ya Sumbula, hilo duara kubwa ni kumbunga cha The Great Red Spot / picha ilipigwa na voyager 1
Chombo cha Voyager 1 kikiwa na dada'ake Voyager 2 viliweza kupokea mawimbi ya radio kutoka kwenye radi zilizokuwa zinapiga kwenye sayari ya Zohali. Wanasayansi waliweza kubadilisha mawimbi hayo kuwa sauti na unaweza ukasikiliza hapo chini kwenye hiyo video.


Hii ni picha ya pete za kwenye sayari ya Zohali iliyopigwa na Voyager 2 tarehe 23/08/1983, kutoka umbali wa maili milioni 2 (kilomita milioni 3.3). Pete za kwenye sayari ya Zohali ni mchanganyiko wa mapande makubwa ya mawe, vumbi, pamoja na barafu ambapo wanasayansi wanaamini ni mwezi ulio pasuliwa na kani kubwa ya uvutano ya kwenye sayari hiyo.

Hii-ni-picha-ya-pete-za-kwenye-sayari-ya-Zohali-iliyopigwa-na-Voyager-2
Muonekano wa karibu wa pete za kwenye sayari ya Zuhula / picha ilipigwa na voyager 2
Hii picha ilipigwa na Voyager 1 tarehe 16/11/1980, siku nne baada ya chombo hicho kupita karibu na sayari hiyo, ili kupata muonekano mzuri wa sayari hiyo pamoja na pete zake zinazoizunguka. Picha hii ilipigwa umbali wa maili milioni 3.3 (kilomita milioni 5.3) kutoka kwenye sayari hiyo.

Hii-picha-ilipigwa-na-Voyager-1-ili-kupata-muonekano-mzuri-wa-sayari-ya-Zuhula
Sayari ya Zuhula ikionekana kwa juu pamoja na pete zake / picha ilipigwa na voyager 1
Hii ni picha ya sayari ya tisa kutoka kwenye Jua, ilipigwa na Voyager 2 wakati ikipita karibu na sayari hiyo, mwezi Januari mwaka 1986.

Hii-ni-picha-ya-sayari-ya-tisa-kutoka-kwenye-Jua
Muonekano wa sayari ya Uranus, ambayo ni ya tisa kutoka kwenye Jua / picha ilipigwa na voyager 2
Voyager 2 ndicho kilikuwa chombo cha kwanza kupiga picha ya sayari ya Kausi tarehe 20/08/1989, wakati chombo hicho kikiwa umbali wa maili milioni 4.4 (kilomita milioni 7) kutoka kwenye sayari hiyo.

Voyager-2-ndicho-kilikuwa-chombo-cha-kwanza-kupiga-picha-ya-sayari-ya-Kausi
Muonekano wa sayari ya kausi / picha ilipigwa na voyager 2
Hii ni picha ya mwisho ambayo ilipigwa na Voyager 1, wakati chombo hicho kwa mara ya kwanza kikiondoka kwenye mfumo wetu wa Jua (Our Solar System) na kuingia kwenye anga ya ndani zaidi huko inayofahamika kama Interstellar Space. Picha hiyo ilipigwa umbali wa maili bilioni 4 kutoka Duniani, na hicho kidoti kidogo kilichooneshewa mshale mwekundu ni Dunia yetu sisi, humo ndimo upo wewe sasa hivi, unaposoma makala hii, na ndipo nyumbani kwako palipo na binadamu wote ikiwamo na wanyama wanapatikana humo, kila kitu ulichowahi sikia, kila mwanadamu aliyeishi, waliofariki, furaha zote, na maumivu yote, mambo yote unayosikia kila siku, mashujaa na magaidi, wagunduzi, wafalme na watumishi, serikali, wapenzi, matumaini, kila mama, kila baba, walimu, wanasiasa wala rushwa, watu mashuhuri, madikteta, watakatifu, wazini katika historia pamoja na viumbe vyote, vinapatikana ndani ya kidoti hicho kidogo." alinukuliwa Carl Sagan akiizungumzia picha hii mwaka 1994.

kidoti-kidogo-kilichooneshewa-mshale-mwekundu-ni-Dunia-yetu-sisi
Hicho kidoti kilichooneshewa mshale mwekundu ni Dunia yetu / picha hii ilipigwa na Voyager 1
Hiyo nyota iliyo katikati inaitwa AC + 79 3888, au Gliese 445, iliyopo umbali wa miaka ya mwanga 17.6 kutoka Duniani. Voyager 1 ni chombo ambacho mpaka kufikia sasa tayari kimeshachochola kutoka kwenye mfumo wetu wa Jua (Our Solar System), na kinaelekea kwenye nyota hiyo ilipo, inasemekana ndani ya miaka 40,000 ijayo, Voyager 1 kitakuwa karibu kabisa na nyota hiyo.

Hiyo-nyota-iliyo-katikati-inaitwa-AC-+-79-3888,-au-Gliese-445
Muonekano wa nyota ya Gliese 445 / Picha hii ilipigwa na Samuel Oschin Telescope
Kidokezo: Mwanga ndiyo kitu chenye spidi kali kuliko vyote ulimwenguni, hivyo vitu vikubwa au safari ndefu za anga ya nje zinapimwa kwa spidi ya mwanga.

Tuandikie maoni yako kuhusu chapisho hili kwenye ukurasa wetu wa Facebook, bila kusahau kusubscribe channel yetu ya YouTube kwa habari, makala, na mambo mengi sana yanayotokea kila siku.INAYOTAZAMWA SASA: ANGALIA MWANAMKE ALIYEJIBADILI KUWA MWEUSI KUTOKANA NA KILE ANACHOSEMA KUWA ANAPENDA RANGI YA WASICHANA WEUSI

SOMA ZAIDI
Andrew Komba

Ghana Kuzianza Mbio Za Anga Ya Nje Afrika

Ghana-Kuzianza-Mbio-Za-Anga-Ya-Nje-Afrika


Satelaiti ya kwanza kutoka Ghana iliyorushwa angani mwezi wa sita mwaka huu 2017 imenza kufanya kazi sasa.

Satelaiti hiyo inayofahamika kama GhanaSat-1, ilitengenezwa na wahandisi watatu kutoka chuo kikuu cha All Nations University (ANUC) ambao walipatiwa msaada wa vifaa, na mafunzo kutoka kwa shirika la masuala ya anga ya nje Japani (JAXA).

Roketi za kampuni ya Space X, kutoka nchini Marekani zilitumika kuisafiri satelaiti hiyo kuelekea kwenye kituo cha kimataifa cha anga ya nje (International Space Station), kisha ikaachiliwa kuanza kuzunguka anga ya Ghana.

Satelaiti hiyo inatarajiwa kuanza kutuma taarifa mbali mbali za mabadiliko ya hali ya hewa pembezoni mwa fukwe na nchini Ghana, pia itatumika kwa ajili ya tafiti zingine mbali mbali zitakazokuwa zikifanyika kwenye maabara ya chuoni hapo.

Licha ya kupata msaada mkubwa kutoka shirika la anga ya nje Japani (JAXA), pia serikali ya nchini humo walitoa pongezi kubwa kwa wahandisi hao watatu Benjamini Bonsu, Ernest Teye, na Joseph Quansah, ambao waliweza kuiunda satelaiti hiyo.

Benjamini-Bonsu,-Ernest-Teye,-na-Joseph-Quansah,-ambao-waliweza-kuiunda-satelaiti-hiyo


Endelea kuwa nasi kwa ku like ukurasa wetu wa Facebook pia usisahau kutoa maoni yako kuhusu chapisho hili na shirikisha na wengine.


ANGALIA HII VIDEO: Mambo 10 usiyofahamu kuhusu ulimwengu

SOMA ZAIDI
Andrew Komba

Hili Ndilo Eneo Ambalo Litaangamia Kama Dar es Salaam, Ikilipuliwa Na Nuklia

By  

Hili-Ndilo-Eneo-Ambalo-Litaangamia-Kama-Dar-es-Salaam,-Ikilipuliwa-Na-Nuklia


Hivi ushawahi kujiuliza nini kitatokea kama bomu la nuklia lenye uzito wa tani 50,000 likidondoshwa katikati ya jiji la Dar es Salaam. Leo tutakwenda kupata majibu kupitia tovuti inayoitwa nuclearsecrecy ambayo inakupa uwezo wa kulipua mji wowote kwa nuklia na kuweza kufahamu maafa yatakayo sababishwa na mlipuko huo.

Tukirudi kidogo kwenye historia ya silaa za nuklia kwa ufupi, kwa mara ya kwanza zilitambulishwa na jeshi la Marekani kwenye vita ya pili ya Dunia, ambapo mabomu mawili ya atomiki yaliyofahamika kwa majina ya utani kama Fat Boy na Little Boy yalidondoshwa huko Japani na kugharimu maisha ya watu 129,000 katika mji wa Hiroshima na Nagasaki na kupelekea mwisho wa vita hiyo.

Tangu hapo silaa hizo zilianza kuonekana kama ndiyo kinga dhabiti kwa mataifa makubwa ambapo Marekani na Urusi walianza kushindana vikali kwa kutengeneza mabomu yenye uwezo mkubwa sana zaidi ya yale yaliyotupwa kule Japani.

Mwaka 1961 Urusi waliibuka kidedea kwa kutengeneza bomu kubwa kuliko yote kuwahi kutengenezwa na binadamu, bomu hilo ambalo liliitwa Tsar Bomba lilikuwa na uzito wa tani 50,000 majaribio yake yalitishia Dunia nzima hivyo Marekani waliamua kuingia makubaliano na Urusi ili kusitisha majaribio mengine ya silaa hizo kali.

Leo nitafanya majaribio kupitia tovuti ya nuclearsecrecy ambayo itatupatia majawabu ya nini kitatokea kama Tsar Bomba likidondoshwa katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Leo-tutafanya-majaribio-kupitia-tovuti-ya-Nuclear-Secrecy-ambayo-inakupa-uwezo-wa-kulipua-sehemu,-jiji-au-nchi-yoyote-ile-Duniani-kwa-bomu-la-nuklia.

Hebu fikiria kama vita ya tatu ya Dunia inatokea leo hii harafu jeshi letu la Tanzania linakuwa upande wa nchi ambazo zinapingana na urusi, halafu pale makao makuu ya amiri jeshi mkuu wa Urusi (Kremlin) wakaamua kuzilipua nchi zote za Afrika ambazo zipo upande tofauti na Urusi ikiwemo na nchi yetu Tanzania, na wakaanza na jiji letu la Dar es Salaam. Hakuna anayefahamu nini kitatokea lakini kupitia hii tovuti ya nuclearsecrecy tutaweza kufahamu kitakachotokea kama bomu moja la Tsar Bomba likitupwa kwenye kitovu cha jiji la Dar es Salaam.

Hapa tutakwenda kuchagua jiji la Dar es Salaam, na aina ya bomu ni Tsar Bomba lenye uzito wa tani 50,000.

Hapa-tutakwenda-kuchagua-jiji-la-Dar-es-Salaam,-na-aina-ya-bomu-ni-Tsar-Bomba-lenye-uzito-wa-tani-50,000.

Zaidi ya watu milioni 2 watakufa papo hapo huku wengine takribani 200,000 wakiachwa ni majeruhi. Kulingana na hii ramani inavyoonesha bomu hilo litachukua eneo kubwa sana si Dar es Salaam pekee bali na maeneo yalikuwa karibu.

eneo-lenye-duara-jekundu-ndipo-mionzi-mikali-itakapoanzia
eneo lenye duara jekundu ndipo mionzi mikali itakapoanzia
Bomu hilo litaacha shimo lenye urefu wa futi 11,000 kwenda chini, na upana wa kilometa 6.

Bomu-hilo-litaacha-shimo-lenye-urefu-wa-futi-11000-kwenda-chini,-na-upana-wa-kilometa-6.
mfano wa shimo ambalo bomu la nuklia linaweza kuchimba
Sehemu hiyo itakuwa na mionzi mikali sana, ambapo asilimia 90% ya eneo lote litakuwa si rafiki tena kukaliwa na viumbe hai kwa zaidi ya miaka 1000 kutokana na mionzi hiyo ambayo inakuwa na madhara makubwa sana kwenye miili ya viumbe hai.

asilimia-90-ya-watu-waliokuwa-kwenye-eneo-hilo-watakufa-ndani-ya-masaa-kadhaa.
asilimia 90% ya watu waliokuwa kwenye eneo la njano watakufa kwa miale mikali

Mlipuko mkali wa moto utafuata na kuweza kuunguza kila kitu kilichomo ndani ya eneo hilo.

Kitu-chochote-kilichomo-kwenye-eneo-hilo-kitayeyuka-kutokana-na-moto-mkali-utakaotokana-na-mlipuko-huo-mkubwa.
Picha ya mlipuko wa bomu la nuklia kwenye majaribio
Upepo mkubwa wenye nguvu zaidi ya kimbunga utafuata na kupeperusha majengo yote makubwa ikiwemo na vitu vingine vyote katika eneo hilo na hakuna kitu hata kimoja ambacho kitasalia hata kijiti hakitobaki kila kitu kitasambaratishwa.

Majengo-yote-makubwa-ikiwemo-na-idadi-kubwa-ya-watu-vitapeperushwa-na-msukumo-mkubwa-wa-mlipuku-wa-upepo-na-hakuna-kitu-ambacho-kitasalia-hata-kijiti-hakitobaki-kila-kitu-kitasambaratishwa-na-kubaki-uwanja-tambalale.
Picha ya majengo yaliyoharibika huko Japani baada ya mlipuko wa nuklia
Watu watakao kuwa kwenye eneo lenye rangi ya njano (angalia ramani) wataathirika na mionzi mikali ya joto, ambapo sehemu kubwa ya miili yao itakuwa imeungua sana mpaka ngozi ya ndani nyeupe kutokeza na kutokana na kuungua huko vibaya hata mishipa ya maumivu itakuwa imeungua hivyo hawatosikia maumivu yoyote na hawatoweza kuishi kwa muda mrefu.

Watu-watakao-kuwa-kwenye-eneo-hilo-wataathirika-na-mionzi-mikali-ya-joto,-ambapo-sehemu-kubwa-ya-miili-yao-itakuwa-imeungua-sana
Mmoja kati ya waasilika wa miale mikali ya nuklia huko Japani
Eneo lenye duara jekundu ndipo mionzi mikali na hatari itakapoanzia kusambaa na kuelekea kwenye maeneo mengine kama Zanzibar, na hakuna kiumbe chochote ambacho kitaweza kupona kama kikikutana na mionzi hiyo.

eneo-lenye-duara-jekundu-ndipo-miale-mikale-itakapoanzia
Mionzi mikali itaanzia hapo kwenye eneo jekundu na kusambaa kwingineko
Kulingana na matokeo hayo zaidi ya watu milioni 2 watapoteza maisha papo hapo, ndani ya jiji la Dar na mikoa mingine iliyokuwa karibu na kuacha majanga makubwa sana kwenye jiji hilo kama kutoweza kukaliwa tena kwa zaidi ya miaka 1000 ijayo.

Hivyo ndivyo tovuti ya nuclearsecrecy inavyotuonesha jinsi bomu la Tsar Bomba lililotengenezwa miaka ya 60 kutoka umoja wa nchi za kijamaa USSR, ambavyo lingeweza kuliangamiza jiji lote la Dar es Salaam na hakuna kiumbe ambacho kingeweza kusalimika.

Sasa kama bomu lililotengenezwa miaka 57 iliyopita linaweza kuangamiza jiji zima, je hayo yaliyokuwa kwenye maghala yao sasa hivi yatakuwaje?

Pia unaweza ukaingia kwenye tovuti hiyo hapa nuclearsecrecy na kujaribu kulipua sehemu zingine kisha ukatoa maoni yako hapo chini.

ANGALIA HII VIDEO: Mambo 5 yanayomfanya mwanaume awe na mvuto zaidi

SOMA ZAIDI