Andrew Komba

China Kutumia Kompyuta Kumtambua Muhalifu Kabla Hajafanya Tukio

China-Kutumia-Kompyuta-Kumtambua-Muhalifu-Kabla-Hajafanya-Tukio


Serikali ya China wanaandaaa mkakati wa kuanza kutumia kompyuta zenye teknolojia ya hali ya juu inayofahamika kama Artificial Intelligence, ili kusaidia jeshi la polisi kuwatambua wahalifu kupitia matendo yao wanapokuwa kwenye jamii kabla hawajafanya matukio. Teknolojia ya Artificial Intelligence inaipa uwezo mkubwa kompyuta wa kuweza kuchanganua mambo na kutolea maamuzi yenyewe pasipo kuwepo mtu kuiamuru.

Kwa-mfano,-mtu-akienda-kununua-kisu-hato-tiliwa-mashaka-na-kompyuta-hiyo,-ila-mtu-huyo-huyo-akirudi-tena-kununua-nyundo-na-gunia

Kompyuta hizo zitakuwa zikifanya kazi na zaidi ya kamera milioni 176 zilizofungwa kwenye sehemu mbali mbali nchini humo. Kamera zitakuwa zikichukua matukio ya mtu kisha kompyuta itaweza kuchanganua matendo yake na kuweza kumfahamu huyo mtu kama ni muhalifu au si muhalifu na kama ni muhalifu basi kompyuta itatoa taarifa polisi haraka sana.

Kwa mfano, mtu akienda kununua kisu dukani hato tiliwa mashaka na kompyuta hiyo, ila mtu huyo huyo akirudi tena kununua nyundo na gunia, kompyuta itamtilia mashaka na polisi watapewa taarifa haraka sana. Teknolojia hiyo pia itakuwa na uwezo wa kuchunguza mwenendo wa mtu kama jinsi anavyoongea, kutembea na itaweza kumtambua mtu hata awe katika kundi la watu.

Tuandikie maoni yako kuhusu chapisho hili kwenye ukurasa wetu wa Facebook, pia usisahau kusubscribe channel yetu ya YouTube kwa video zilizochambuliwa kwa undani zaidi juu ya masuala yanayotokea Duniani.

INAYOTAZAMWA SASA: KITANDA HIKI KINAWEZA BADILIKA KUWA SEHEMU YA KUANGALIZIA SINEMA