Andrew Komba

Ghana Kuzianza Mbio Za Anga Ya Nje Afrika

Ghana-Kuzianza-Mbio-Za-Anga-Ya-Nje-Afrika


Satelaiti ya kwanza kutoka Ghana iliyorushwa angani mwezi wa sita mwaka huu 2017 imenza kufanya kazi sasa.

Satelaiti hiyo inayofahamika kama GhanaSat-1, ilitengenezwa na wahandisi watatu kutoka chuo kikuu cha All Nations University (ANUC) ambao walipatiwa msaada wa vifaa, na mafunzo kutoka kwa shirika la masuala ya anga ya nje Japani (JAXA).

Roketi za kampuni ya Space X, kutoka nchini Marekani zilitumika kuisafiri satelaiti hiyo kuelekea kwenye kituo cha kimataifa cha anga ya nje (International Space Station), kisha ikaachiliwa kuanza kuzunguka anga ya Ghana.

Satelaiti hiyo inatarajiwa kuanza kutuma taarifa mbali mbali za mabadiliko ya hali ya hewa pembezoni mwa fukwe na nchini Ghana, pia itatumika kwa ajili ya tafiti zingine mbali mbali zitakazokuwa zikifanyika kwenye maabara ya chuoni hapo.

Licha ya kupata msaada mkubwa kutoka shirika la anga ya nje Japani (JAXA), pia serikali ya nchini humo walitoa pongezi kubwa kwa wahandisi hao watatu Benjamini Bonsu, Ernest Teye, na Joseph Quansah, ambao waliweza kuiunda satelaiti hiyo.

Benjamini-Bonsu,-Ernest-Teye,-na-Joseph-Quansah,-ambao-waliweza-kuiunda-satelaiti-hiyo


Endelea kuwa nasi kwa ku like ukurasa wetu wa Facebook pia usisahau kutoa maoni yako kuhusu chapisho hili na shirikisha na wengine.


ANGALIA HII VIDEO: Mambo 10 usiyofahamu kuhusu ulimwengu