Andrew Komba

Hivi Ndivyo Kompyuta Zitakavyotawala Binadamu Duniani

Hivi-Ndivyo-Kompyuta-Zitakavyotawala-Binadamu-Duniani

Nadhani wengi wetu tutakuwa tumeshawahi kuangalia filamu maarufu kama Terminator iliyochezwa na Arnold, na zingine nyingi ambazo zenye maudhui ya kuonesha jinsi kompyuta zenye weledi wa hali ya juu zikiiteka Dunia na kutaka kuangamiza binadamu wote. Kutokana na kukua kwa kasi kwa teknolojia ya kompyuta zenye weledi wa hali ya juu (Artificial Intelligence) wanasayansi kutoka sehemu mbali mbali Duniani wanaamini ndani ya miaka 100 kutokea sasa, Dunia yetu itakuwa imetawaliwa na kompyuta hizo zenye weledi wa hali ya juu ambapo hazitakuwa tofauti kimaumbo na binadamu ila kwa akili zitakuwa zimetuzidi sana.

Dunia-yetu-itakuwa-imetawaliwa-na-kompyuta-hizo-zenye-weledi-wa-hali-ya-juu
Muonekano wa roboti zenye weledi wa hali ya juu kiakili / picha kutoka kwenye filamu ya iRobot
Hivi karibuni yaliyoteka malumbano makali sana kati ya mabilionea wawili Mark Zuckerberg ambaye ni muanzilishi wa mtandao kijamii wa Facebook, pamoja na mmiliki wa kampuni ya Tesla, Elon Musk, mabishano yao makali ambayo yalikuwa ni kuhusu madhara ambayo yanaweza kuletwa kutokana na kuziboresha kompyuta kiuwezo wa akili, ambapo bwana Elon Musk akipingana na muendelezo wa teknolojia hiyo ya Artificial Intelligence wakati Mark Zuckerberg akisema haina madhara kwani tangu kuzinduliwa kwake teknolojia hiyo imeleta msaada mkubwa sana kwenye taasisi na mashirika mbali mbali mfano kusaidia kufanya upasuaji mahospitalini kwa wagonjwa na kwenye nyanja ya magari yanayojiendesha yenyewe. Mjadala huo dhidi ya mabilionea hao wawili uliishia kwa Elon Musk kumwambia Mark Zuckerberg ufahamu wake dhidi ya teknolojia hiyo ni mdogo sana hivyo hawezi tambua madhara yake.

Mark-Zuckerberg-na-Elon-Musk-wamekuwa-wakibishana-vikali-kuhusu-Artificial-Intelligence
Kushoto ni Mark Zuckerberg wa Facebook na kulia ni Elon Musk wa Tesla
Artificial Intelligence ni nini? Artificial Intelligence ni tawi la sayansi ya kompyuta ambapo dhumuni kubwa la teknolojia hiyo ni kuunda kompyuta zenye uwezo mkubwa wa kiakili kama kutatua matatizo mbali mbali pasipo kutegemea binadamu, kutafakari, kujifunza, kupanga mikakati, kujitambua zenyewe pamoja na uwezo wa kufanya kazi kama binadamu.

Mpaka kufikia sasa baadhi ya kazi nyingi za viwandani kwenye nchi zilizoendelea zinafanywa na maroboti mfano uundwaji wa magari, na upakiaji wa vitu kwenye viwanda vikubwa. Inategemewa ndani ya miongo miwili ijayo kazi nyingi zitachukuliwa na maroboti na kuacha idadi kubwa ya watu bila kazi.

kazi-nyingi-zitachukuliwa-na-maroboti
Sehemu kubwa ya nguvu kazi itachukuliwa na maroboti
Mwanasanyansi Stephen Hawking na Elon Musk wamekuwa mstari wa mbele kupinga muendelezo wa teknolojia ya Artificial Intelligence, huku hofu kubwa iliyokuwepo kwa wanasayansi hao pamoja na mijadala mikali inayofanywa na wataalam wa masuala ya teknolojia Duniani kote, ni kwamba kukua kwa kasi kwa teknolojia hiyo kunaweza kusababisha mwisho wa Dunia, ambapo hapo baadae kompyuta zitakuwa na uwezo mkubwa wa kiakili hivyo kututawala sisi binadamu kama binadamu wanavyotawala wanyama wengine majumbani kama mbwa, ng'ombe n.k.

wanadamu-watakuwa-ni-watumwa-wa-maroboti
Picha sanifu ya Artificial Intelligence
Mwanzoni mwa mwaka huu kampuni ya Facebook walilazimika kuzima moja kati ya kompyuta iliyokuwa na uwezo wa Artificial Intelligence, sakata hilo lilitokea baada ya kompyuta hiyo kuweza kutengeneza lugha yake yenyewe ambayo hakuna binadamu aliyekuwa anaielewa lugha hiyo, hivyo wasiwasi mkubwa ulitanda kwamba huenda kompyuta hiyo ikiendelea kuachwa basi inaweza ikatengeneza lugha ambazo zikatumika katika mawasiliano dhidi ya maroboti na binadamu hatutoweza kuzielewa. Tahadhari kubwa ilichukuliwa na kompyuta hiyo ilizimwa haraka sana.

Tuandikie maoni yako kuhusu chapisho hili kwenye ukurasa wetu wa Facebook, bila kusahau kusubscribe channel yetu ya YouTube kwa habari, makala, na mambo mengi sana yanayotokea kila siku.INAYOTAZAMWA SASA: JE, UNATAKA KUTENGENEZA KIPATO CHA ZIADA MTANDAONI TEMBELEA TOVUTI HIZI TANO KUFAHAMU