Andrew Komba

Vifahamu Vyombo Pekee Kuwahi Kutengenezwa na Binadamu Ambavyo Vimetoka Nje Ya Mfumo Wetu Wa Jua


Vifahamu-Vyombo-Pekee-Kuwahi-Kutengenezwa-na-Binadamu-Ambavyo-Vimetoka-Nje-Ya-Mfumo-Wetu-Wa-Jua


Mwaka 1977 shirika la NASA kutoka nchini Marekani ambalo linahusika na uundaji wa ndege za kisasa pamoja na safari za anga ya nje, walitengeneza vyombo viwili vilivyofahamika kama Voyager 1 na 2 ambavyo viliundwa kwa ajili ya kufanya safari za ndani zaidi kwenye anga la nje.

Chombo cha kwanza kuruka kilikuwa ni Voyager 2, ambacho kilirushwa tarehe 20/08/1977 na kufuatia kingine kilichoitwa Voyager 1, ambacho kilirushwa tarehe 05/09/1977. Vyombo hivyo viwili ambavyo kila kimoja kilirushwa kwenye njia yake, huku Voyager 1 kilitakiwa kufikia sayari ya Sumbula na Zohari, kabla ya Voyager 2.

Chombo-cha-kwamza-kuruka-kilikuwa-ni-Voyager-2
Roketi ikionekana pichani kuipeleka Voyager 2 angani
Pichani hapo chini ni moja kati ya kamera ambayo imefungwa kwenye chombo cha Voyager 2, ikioneshwa na Richard Laeser ambaye ni mkurugenzi wa safari za Voyager 1 na 2.

Pichani-hapo-chini-ni-moja-kati-ya-kamera-ambayo-imefungwa-kwenye-chombo-cha-Voyager-2,-ikioneshwa-na-Richard-Laeser-ambaye-ni-mkurugenzi-wa-safari-za-Voyager-1-na-2
Pichani mkurugenzi wa safari za Voyager 1 na 2 Richard Laeser akizungumzia juu ya kamera iliyofungwa kwenye voyager 2
Wahandisi wakiunda antena kubwa ambayo ilikwenda kutumika kwenye moja kati ya vyombo vya Voyager 1 na 2.

Wahandisi-wakiunda-antena-kubwa-ambayo-ilikwenda-kutumika-kwenye-moja-kati-ya-vyombo-vya-Voyager-1-na-2
Pichani wahandisi wakiunda moja kati ya antena za kwenye Voyager
Voyager 1 na 2 vimewekewa rekodi mbili za dhahabu ambazo zinasauti mbali mbali kutoka Duniani, ikiwemo sauti za salamu za watu kutoka lugha 60 tofauti tofauti, miziki ya tamaduni mbali mbali, sauti za watu wakiongea, wanyama, magari, ndege na vyombo vingine vya usafiri.

Voyager-1-na-2-vimewekewa-rekodi-mbili-za-dhahabu-ambazo-zinasauti-mbali-mbali-kutoka-Duniani
Pichani rekodi mbili za dhahabu ambazo zimebeba sauti na picha mbali mbali kuhusu Dunia yetu
Hii ni picha ya kwanza ambayo ilipigwa na Voyager 1 tarehe 18/09/1977 wakati chombo hicho kilipokuwa umbali wa maili milioni 7.25 (kilomita milioni 11.66) kutoka Duniani.

Hii-ni-picha-ya-kwanza-ambayo-ilipigwa-na-Voyager-1
Picha ya muonekano wa Dunia na mwezi iliyopigwa na voyager 1
Hii picha ilipigwa tarehe 05/03/1979 wakati Voyager 1 ikiikaribia sayari ya Sumbula.

Hii-picha-ilipigwa-na-Voyager-1-wakati-ikiikaribia-sayari-ya-Sumbula
Voyager 1 ikiikaribia sayari ya Sumbula / picha ilipigwa na voyager 1
Kati ya mwezi Januari na Februari mwaka 1979, chombo cha Voyager 1 kilisogea kwa ukaribu kwenye sayari ya Sumbula na kuweza kunasa picha kadhaa ambazo zilionesha uso wa sayari hiyo kwa ukaribu, ikiwamo mawingu yake ya gesi pamoja na kimbunga kikubwa sana kwenye mfumo wetu wa Jua (Our Solar System). Kimbunga hicho kinafahamika kama The Great Red Spot ambacho upepo wake unavuma maili 400 kwa saa huku kikiwa kinazunguka kwenye sayari hiyo, na ukubwa wa kimbunga hicho ni sawa na Dunia zetu tatu.

Kimbunga-hicho-kinafahamika-kama-The-Great-Red-Spot
Muonekano wa karibu wa sayari ya Sumbula, hilo duara kubwa ni kumbunga cha The Great Red Spot / picha ilipigwa na voyager 1
Chombo cha Voyager 1 kikiwa na dada'ake Voyager 2 viliweza kupokea mawimbi ya radio kutoka kwenye radi zilizokuwa zinapiga kwenye sayari ya Zohali. Wanasayansi waliweza kubadilisha mawimbi hayo kuwa sauti na unaweza ukasikiliza hapo chini kwenye hiyo video.


Hii ni picha ya pete za kwenye sayari ya Zohali iliyopigwa na Voyager 2 tarehe 23/08/1983, kutoka umbali wa maili milioni 2 (kilomita milioni 3.3). Pete za kwenye sayari ya Zohali ni mchanganyiko wa mapande makubwa ya mawe, vumbi, pamoja na barafu ambapo wanasayansi wanaamini ni mwezi ulio pasuliwa na kani kubwa ya uvutano ya kwenye sayari hiyo.

Hii-ni-picha-ya-pete-za-kwenye-sayari-ya-Zohali-iliyopigwa-na-Voyager-2
Muonekano wa karibu wa pete za kwenye sayari ya Zuhula / picha ilipigwa na voyager 2
Hii picha ilipigwa na Voyager 1 tarehe 16/11/1980, siku nne baada ya chombo hicho kupita karibu na sayari hiyo, ili kupata muonekano mzuri wa sayari hiyo pamoja na pete zake zinazoizunguka. Picha hii ilipigwa umbali wa maili milioni 3.3 (kilomita milioni 5.3) kutoka kwenye sayari hiyo.

Hii-picha-ilipigwa-na-Voyager-1-ili-kupata-muonekano-mzuri-wa-sayari-ya-Zuhula
Sayari ya Zuhula ikionekana kwa juu pamoja na pete zake / picha ilipigwa na voyager 1
Hii ni picha ya sayari ya tisa kutoka kwenye Jua, ilipigwa na Voyager 2 wakati ikipita karibu na sayari hiyo, mwezi Januari mwaka 1986.

Hii-ni-picha-ya-sayari-ya-tisa-kutoka-kwenye-Jua
Muonekano wa sayari ya Uranus, ambayo ni ya tisa kutoka kwenye Jua / picha ilipigwa na voyager 2
Voyager 2 ndicho kilikuwa chombo cha kwanza kupiga picha ya sayari ya Kausi tarehe 20/08/1989, wakati chombo hicho kikiwa umbali wa maili milioni 4.4 (kilomita milioni 7) kutoka kwenye sayari hiyo.

Voyager-2-ndicho-kilikuwa-chombo-cha-kwanza-kupiga-picha-ya-sayari-ya-Kausi
Muonekano wa sayari ya kausi / picha ilipigwa na voyager 2
Hii ni picha ya mwisho ambayo ilipigwa na Voyager 1, wakati chombo hicho kwa mara ya kwanza kikiondoka kwenye mfumo wetu wa Jua (Our Solar System) na kuingia kwenye anga ya ndani zaidi huko inayofahamika kama Interstellar Space. Picha hiyo ilipigwa umbali wa maili bilioni 4 kutoka Duniani, na hicho kidoti kidogo kilichooneshewa mshale mwekundu ni Dunia yetu sisi, humo ndimo upo wewe sasa hivi, unaposoma makala hii, na ndipo nyumbani kwako palipo na binadamu wote ikiwamo na wanyama wanapatikana humo, kila kitu ulichowahi sikia, kila mwanadamu aliyeishi, waliofariki, furaha zote, na maumivu yote, mambo yote unayosikia kila siku, mashujaa na magaidi, wagunduzi, wafalme na watumishi, serikali, wapenzi, matumaini, kila mama, kila baba, walimu, wanasiasa wala rushwa, watu mashuhuri, madikteta, watakatifu, wazini katika historia pamoja na viumbe vyote, vinapatikana ndani ya kidoti hicho kidogo." alinukuliwa Carl Sagan akiizungumzia picha hii mwaka 1994.

kidoti-kidogo-kilichooneshewa-mshale-mwekundu-ni-Dunia-yetu-sisi
Hicho kidoti kilichooneshewa mshale mwekundu ni Dunia yetu / picha hii ilipigwa na Voyager 1
Hiyo nyota iliyo katikati inaitwa AC + 79 3888, au Gliese 445, iliyopo umbali wa miaka ya mwanga 17.6 kutoka Duniani. Voyager 1 ni chombo ambacho mpaka kufikia sasa tayari kimeshachochola kutoka kwenye mfumo wetu wa Jua (Our Solar System), na kinaelekea kwenye nyota hiyo ilipo, inasemekana ndani ya miaka 40,000 ijayo, Voyager 1 kitakuwa karibu kabisa na nyota hiyo.

Hiyo-nyota-iliyo-katikati-inaitwa-AC-+-79-3888,-au-Gliese-445
Muonekano wa nyota ya Gliese 445 / Picha hii ilipigwa na Samuel Oschin Telescope
Kidokezo: Mwanga ndiyo kitu chenye spidi kali kuliko vyote ulimwenguni, hivyo vitu vikubwa au safari ndefu za anga ya nje zinapimwa kwa spidi ya mwanga.

Tuandikie maoni yako kuhusu chapisho hili kwenye ukurasa wetu wa Facebook, bila kusahau kusubscribe channel yetu ya YouTube kwa habari, makala, na mambo mengi sana yanayotokea kila siku.INAYOTAZAMWA SASA: ANGALIA MWANAMKE ALIYEJIBADILI KUWA MWEUSI KUTOKANA NA KILE ANACHOSEMA KUWA ANAPENDA RANGI YA WASICHANA WEUSI