Andrew Komba

Facebook wakubali kwamba matumizi ya mtandao huo yana madhara kwa maisha ya kila siku

Facebook-wakubali-kwamba-matumizi-ya-mtandao-huo-yana-madhara-kwa-maisha-ya-kila-siku


Mkurugenzi wa tafiti Facebook David Ginsberg na mtaalamu wa utafiti Moira Burke wamekubali kwamba matumizi ya mtandao wa Facebook unamadhara makubwa sana kwenye jamii. Viongozi hao wa ngazi za juu kwenye kampuni hiyo ya Facebook walikubali madhara ya mtandao huo kwenye jamii kutokana na maswali mengi kuwepo dhidi ya madhara ya mtandao huo kwenye jamii.

Katika utafiti uliofanywa, unaonesha kwamba watu wanaotumia mtandao huo kuangalia machapisho ya watu wengine huwa wanakuwa katika hali ya msongo wa mawazo, wakati wale wengine wanaotumia mtandao huo kuchapisha na kuwasiliana na marafiki wanakuwa katika hali ya furaha.

Hii inamaana kwamba kama unatumia muda wako mwingi Facebook kuangalia news feed au ku like machapisho ya watu, lazima utakuja kusumbuliwa na msongo wa mawazo.

Facebook pia walishirikiana na chuo cha Carnegie Mellon katika kutambua zaidi tabia za watu ndani ya mtandao huo, na kugundua "watu wanaotumia mtandao huo kuwasiliana, kutoa maoni, na kuchapisha vitu, huwa ni wale ambao wanafuraha sana, wasiokuwa na msongo wa mawazo." Pia utafiti huo ulionesha kwamba watu wanaotumia dakika 5 kuangalia Profile zao huwa wanajikubali sana tofauti na wale ambao wanaangalia profile za watu wengine.

Tunahitimisha kwa kusema Facebook imetengenezwa maalum kwa kuwasiliana na watu wengine, na ukifanya hivyo ndo inashauliwa na ni nzuri kiafya, ila kama utatumia mtandao huo kivingine basi utakuwa ni mlengwa wa madhara kama msongo wa mawazo, upweke, ambapo si nzuri kiafya.


ANGALIA HII VIDEO: MAKOSA 10 AMBAYO VIJANA WENGI WANAFANYA WAKATI WA USAILI WA KAZI